Kufika Mlima
Kigango kiko kilomita nne kutoka kanisa kuu, juu ya barabara ya murram kupita zahanati. Matatu hufika hadi zahanati asubuhi za Jumapili na si zaidi.
Baada ya mvua kubwa sehemu ya mwisho haipitiki kwa gari. Watu wengi hutembea kwa takriban dakika hamsini.